Wasanii
Orodha ifuatayo ni ya Wasanii wa muziki Tanzania ambao nilibahatika kuongea nao LIVE kwenye simu na kufanya mazungumzo nao kupata uelewa kamili juu ya mahitaji yao katika kazi zao za kisanii za kimuziki na filamu. Wasanii hawa walinifahamisha mambo mengi sana ya manufaa ambayo yalinipa nguvu kubwa na ari ya kiukweli katika ujenzi wa MSOL-AB. Katika kuchambua maoni yao niliona kuna mahitaji ya kufanyiwa kipaumbele:-
- Uzalishaji bora wa muziki na filamu na uelewa wa hakimiliki katika nyanja hizo na namna ya kudhibiti uharamia katika kazi zao
- Uelewa wa kupata masoko katika kazi zao na uendeshaji bora wa kazi kama Wajasiriamali
- Uzalishaji na uuzaji wa kazi za kisanii wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa
Majina ya Wasanii, tarehe kamili tuliyoongea na maoni yao. Nawashukuru sana wasanii hawa kwa kunipa muda wao kuongea na mimi. Hawa ndio walionipa nguvu ya kuanzisha Kampuni kubwa kama ya MSOL-AB na moja ya kampuni ya aina yake katika dunia hii katika kuiunganisha dunia kwa kutumia Wasanii na kazi zao za kisanii
- BWANA MISOSI-tel: +255-713......90 na +255-763......55 tarehe 21 machi, 2013. Alifurahia sana ujio wa Kampuni aina hiyo na aliniunga mkono na hakuonyesha uchoyo, akaniunganisha kwa kunipa namba za simu za wengine aliopenda nao kupata habari za MSOL-AB
- HUSSEIN MACHOZI-tel: +255-718......28. Tarehe 21 machi, 2013. Alifurahia sana ujio wa MSOL-AB. Ailitaka kujua kama wakija Sweden kufanya kazi katika kikundi, je,watarekodi pamoja na Wasanii wengine? Jibu ni hapana kila Msanii atakuwa na siku zake pekee yake, labda akitaka kuimba na Msanii mwingine ni ruksa. Alitaka kujua kuhusu chakula. Yeye ni Mwislamu ambaye chakula chake asingependa ale kila kitu. Jibu: Vyakula vyote vitapikwa na Mtaalamu wa mambo ya vyakula vya Kihoteli Mtanzania na atapika chakula cha washiriki kutokana na order ya kila mtu atakavyotaka. "Vigezo na Masharti kuzingatiwa"
- BABU TALE-tel: +255-754......13 na +255-715......46. Tarehe 23 machi, 2013. Aliufurahia sana ujio wa Kampuni aina hiyo yenye kutoa ELIMU kwa vile wengi watafaidika sana kwa kuwatoa walipo sasa hivi. Aliuliza kama kulikuwa na mpango wowote wa kupewa Elimu za sheria za muziki au filamu na Elimu ya Masoko kwa viongozi wa Wasanii. Jibu ni kwamba wazo lake tayari limefanyiwa kazi. Kozi zote mbili zipo katika programu za MSOL-AB. Karibu Sweden viongozi wa bendi zote na Bongomovies
- DAYNA-tel: +255-716......00. Tarehe 23 machi, 2013. Aliunga mkono ujio wa MSOL-AB, alikuwa akirudi nyumbani kwenda kulala baada ya kununua chakula jioni hiyo na alinishauri nisikatishwe tamaa na mtu yeyote ni wazo lililokuwa nao ni la manufaa makubwa wasanii wote
- FID Q-tel: +255-713......51. Tarehe 1 aprili, 2013. Alikuwa na shughuli nyingi siku hiyo, lakini baadaya kuweleza mpango wa kuianzisha kampuni aliniunga mkono na akaniomba niendelee na mpango huo ambao utakuwa ni wa manufaa na mwokozi wao
- FELLA (TMK)-tel: +255-713......14. Tarehe 5 aprili, 2013. Alifurahishwa kuliko kawaida aliposikia ujio wa kampuni inayotafuta njia za kuwasaidia Wasanii wa Tanzania katika kujikwamua na hali duni walionayo na alikuwa na hamu ya kuiona MSOL-AB ikifanya vitu vyake kama nilivyoeleza na aliahidi yeye na kikundi chake kuitumia kampuni hii kuwapa Elimu na kuwapa utaalamu wa kisasa katika utengenezaji video za muziki na filamu. Kwa kifupi kazi za kisanii
- DIAMOND PLATZNUMZ nyumbani kwa BABU TALE-tel: +255-769......99. Tarehe 5 aprili, 2013. Aliufurahia sana mpango huo kuwepo kwa MSOL-AB hasa kwa vile mbali ya kufanyiwa kazi zake Msanii pia mtu unapata ELIMU. Ni kitu kizuri sana
- JUMA NATURE (KIROBOTO)-tel: +255-658......08. Tarehe 5 aprili, 2013. Nilianza kumpigia simu saa mbili jioni akasema kwamba nimpigie baadaye kidogo. Baada ya saa nzima nilimpigia tena akaniambia bado yupo bize, nimpigie baada ya saa nzima nyingine maana wakati wote huo alikuwa Studio akirekodi wimbo wake. Baada ya kupita saa nzima kwenye saa tano kamili za usiku nilimpigia tena. Nilipomweleza wazo la kuanzisha MSOL-AB na kazi zake zote kwa kina. Hakuona umuhimu wake na hakuona faida atakayoipata yeye binafsi kutoka MSOL-AB. Alizidi kutoa yake ya moyoni kuwa, ameshaibiwa sana katika maisha yake na watu. Kwa hiyo hakuamini chochote toka kwangu au kwa mtu mwingine yeyote hatamwamini. Mtu pekee anayemwamini ni Mhe. Dr Jakaya Kikwete, Rais wa Tanzania na anaamini ndiye mtu pekee atakayewasaidia Wasanii Tanzania. Hakuna mwingine, kwa heri! Akakata simu! Kwa maoni ya namna hiyo ni changa moto kubwa kwa MSOL-AB katika kuendesha kazi zake. MSOL-AB ilete imani kubwa na imara kwa Wasanii akina Juma Nature wote Tanzania na nchi zote duniani MSOL-AB itakapokuwa ikifanya kazi zake
- FELLA (TMK-Family)-tel: +255-713......14.Tarehe 13 aprili, 2013. Kwa jinsi alivyokuwa amehamasika sana na ujio wa MSOL-AB alitaka ianze kazi zake mara moja ili yeye atume kikundi chake Sweden mara moja kupata ELIMU hiyo. Hata Chegge alipokuja Sweden kuonyesha show zake Mzee Fella alinipigia simu na akinisisitizia kuwa nikutane na Chegge. Nilijitahidi kupata nafasi ya Chegge kukutana na mimi, Mtayarishaji wa show zake alimpa ratiba iliyokuwa finyu sana. Matokeo yake siku aliyotakiwa kuja kuonana na mimi alikuwa tayari akielekea Uwanja wa Ndege kurudi Tanzania. Chegge alinipigia simu ili kuniaga. Hakukuwa na jinsi ila nilimweleza Chegge kuwa tutaonana tu siku zijazo nafasi nyingine ya kuja Sweden ikipatikana
- KEISHA-tel: +255-718......45. Tarehe 15 aprili, 2013. Alipendezwa na ujio wa MSOL-AB na hasa programmu zake zilionyesha kuwa zitawanufaisha sana Wasanii wa Tanzania. Aliomba proct hiyo isiishie njiani, niiendeleze
- MZEE YUSSUFU-tel: +255-714......71. Tarehe 18 aprili, 2013. Alisema kuwa hakuona umuhimu wowote wa kuwa na kampuni kama hiyo, kwani haikuwa na maana kubwa sana katika kazi zake za kisanii wala umuhimu wowote kwake. Kila kitu kwake kipo sawa
- DULLY SYKES-tel: +255-713......60. Sikumbuki tarehe kamaili niliyoongea naye lakini ilikuwa ni kati ya mwezi April au Mei 2013 Dully alikuwa na haraka ya kuelekea kwenye mazishi ya mmoja wa ndugu yake. Aliniomba nijaribu kumpigia tena wakati mwingine
- AY-tel: +255-715......98..........
- CPWAA, OMMY DIMPOZ na ALLY CHOCKY. Wasanii wetu mahiri wa muziki wote hawa walipendezwa na ujio huu wa MSOL-AB na waliunga mkono kwa nguvu zote. ALLY CHOCKY yeye alikwenda mbele zaidi kwa kupendekeza kujengwa Studio nyingine ya MSOL-AB Tanzania, wazo ambalo MSOL-AB imeliweka katika programu zake za mbele. MSOL-AB katika mpangilio wake wa mwanzo ilikuwa ni kuijenga studio hii Dar es salaam Tanzania (Rejea blogg ya Michuzi tarehe 8 septemba, 2010). Kwa kutaka kufahamishwa jinsi namna na sheria za Tanzania zinavyosema kuhusu kufungua kampuni ya kigeni Tanzania. Niliongea na mmoja wa viongozi wakuu wa BASATA (Mr G. Materego). Kitu cha kwanza alichotaka kukijua toka kwangu ni nani aliyekuwa mshirika au aliyekuwa anaifadhili MSOL-AB huko Sweden. Nilimweleza wazi kuwa MSOL haina mshirika wala mfadhili wa aina yeyote, gharama zote zinatoka mikononi mwangu (Mkurugenzi) mimi mwenyewe. Baada ya hapo sijampata tena. Sijui nilichokikosea katika maelezo yangu. Lakini hata hivyo nililifanyia kazi swali lake katika moja ya programu za MSOL-AB kwa kutafuta na kupata washirika badala ya wafadhili nchini Tanzania badala ya Sweden. MSOL-AB inamakubaliano ya ushirika kati yake na Studio moja kubwa Mwanza na bado tunatafuta Studio nyingine mbili Dar es salaam.
Wasanii wa Tanzania sasa ni "Mambo Hadharani". Kupitia MSOL-AB hakuna upendeleo wala ushabiki, hakuna kuonyeshana na kujivunia kununua magari ya gharama kubwa wala kuwa na majumba ya kifahari. Mkali wa kazi katika muziki ama filamu atapatikana kupitia jamii ya dunia itakavyoinunua kazi yake. MSOL-AB ni "Kazi na Elimu. MSOL-AB Ni "Tochi ya Wasanii katika safari yao ndefu katika kufikia mafanikio. Wasanii wa Tanzania pigeni KAZI penye uzia piga KITABU.
MSOL-AB - Is "Work and Education"
MSOL-AB - Is "The Light of artists to their long walk to success"
Peters Mhoja / CEO / MSOL - AB
|