MSOL AB MUSIC STUDIO OF LEARNING

MSOL AB - MUSIC STUDIO OF LEARNING OF SWEDEN Kuanza | MSOL AB | Huduma | Wasanii | Video na muziki | Film | Mgeni Msanii | Mawasiliano | IN ENGLISH


Huduma zetu

Wasanii wa Tanzania "Upele umepata mkunaji"! Ni MSOL-AB.
Kilio cha Wasanii Tanzania kimesikika hadi Sweden. Ni MSOL-AB imesikia kilio chenu.
Music Studio Of Learning Of Sweden AB kifupisho MSOL-AB-Is the Work and Education (Ni Kazi na Elimu). MSOL-AB-Is the light of artists to their long walk for success (Ni tochi ya Wasanii katika safari yao ndefu ya kufikia mafanikio yao kisanii). Kwa muda mrefu Wasanii wa Tanzania wamekuwa wakienda huku na huko kwa nia ya kutangaza kazi zao nchi za nje.
MSOL-AB itakusikiliza wewe msanii unachokihitaji ikufanyie katika kukutangazia kazi zako katika soko la dunia na ndani ya Tanzania.

Shughuli kuu za MSOL-AB ni;-

  1. Kutoa elimu ya Soko (Marketing) ihusuyo miziki/filamu k.m. namna ya kuendesha biashara ya muziki/filamu na jinsi ya kupata soko la ndani na nje ya Tanzania pia kupata malipo yanayostahili zinaponunuliwa kazi za Msanii Mwanamuziki/filamu ndani na nje.
  2. Kutoa elimu ya Sheria Music legislation/film zihusuzo miziki/filamu k.m. namna ya kuandikiana mikataba na jinsi ya kulinda kazi za Msanii Mwanamuziki/Filamu zisiibiwe kwa njia zote ndani na nje ya Tanzania hata kama msanii atakuwa alishakufa kazi zake zitaendelee kulindwa zisitumike kinyume na sheria zisemazokuwa, ni baada ya kupita miaka 70 baada ya kifo cha msanii huyo kazi zake zinaweza kutumiwa na watu wengine kujinufaisha watakavyoona wao. Ningependa nipate ushirikiano wa karibu na COSOTA katika hili.
  3. Kurekodi muziki/filamu kufanya Mixing na Mastering kwa kutumia studio ya kisasa (digitalized). Sehemu hii itachukua muda mrefu na hasa katika musicvideos/film kwa kila mshiriki, ili kila mwanamuziki/msanii asirekodi muziki/filamu yake kwa kuburuzwa na muda kuwa Sweden. Baada ya kukamilika mixing, kutakuwa na jopo la Wataalamu wa muziki/filamu kuijadili na kuichambua vipengele vyake vyote kazi ya kila mhusika (nyimbo zote atakazopendekeza mhusika zitajadiliwa) na baada ya jopo hilo kuridhika na marekebisho yote kufanyika, muziki/filamu inahifadhiwa katika USB na CD/DVD original ili kupelekwa katika hatua zinazofuatazo hapo chini.
  4. Kwa kazi za Mastering-Kwa kutumia Mastering Experts tu. Katika sehemu hii inashauriwa ni vizuri kuwapa wataalamu wa kuifanya kazi hiyo kuliko kuifanya mastering wewe uliyerekodi muziki/filamu, kwa sababu kama utafanya hivyo utayarudia makosa uliyoyafanya wakati wa kurekodi na kumixi na kupendelea kukiweka kitu unachokipenda wewe pekee. La msingi zaidi hapa ni kiutaalamu, ni kwamba kila mtu ana uwezo wake wa kusikia sauti zingine ambazo mtu mwingine hazisikii. Wataalamu hawa wanajua namna ya kulitatua tatizo hilo. Ndiyo maana utakuta tunatofautiana katika kuvutiwa na aina fulani ya miziki duniani.
  5. Kuituma miziki/filamu iliyopitishwa na Wataalamu wa muziki/filamu kwa makubaliano na Mwanamuziki/Msanii mwenyewe kwa matengenezo ya Albamu yake kwa Wasambazaji. Wasambazaji nao wataisikiliza/kuitazama miziki/filamu yote na kutoa ushauri wao kipi kirekebishwe katika kuzitengeneza albamu. Ni zile tu album zitakazoonekana kukidhi kiwango cha dunia na kuwa zinaweza kununulika duniani ndizo watakazozichukua na kuwauzia wateja wao. Wasambazaji hawatakubali kuteremsha hadhi za kampuni zao kwa kuwapelekea wateja wao miziki/filamu zilizo chini ya kiwango. Kila muziki hutumia sekunde 15 tu kwa Wasambazaji kuzisikiliza na kutoa uamuzi. Albamu zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya wateja wao watazitengeneza na kuzisambaza wenyewe. Albamu watazitangaza katika vyombo vyao vya habari zaidi ya elfu moja duniani kote. Mimi pia kwa nafasi yangu nitatembea kila sehemu Sweden na nje ya Sweden kuzitangaza kwa wenyeji wa nchi hizo na Wanadiaspora wenzetu wote.
  6. MSOL-AB pamoja na mwanamuziki/Msanii ambaye hakufikia kiwango cha kutengenezewa albamu yake na Wasambazaji, MSOL itawekeana naye mikataba ya kisheria namna ya kutengeneza albamu hizo kwa watengeneza albamu wengine ambao watakuwa tayari kuchukua jukum hilo la kazi hiyo bila ya kujali kuteremsha hadhi ya Kampuni yao ya kurekodi kazi iliyo chini ya kiwango, kwa makubaliano maalum ya kisheria. Makubaliano kati ya MSOL na Mhusika yatahusu pia kuzileta albamu hizo Tanzania kwa kuzitengeneza upya miziki/filamu kwenye Audio CD na cassette, VCD na DVD kwa ajili ya soko la ndani lakini kwa masharti ya kulinda uthamani wa kampuni yetu, tutakataza kutumia jina la MSOL kwa namna yoyote. Kwa vile mwanamuziki mwenyewe atakuwa amepata elimu ya soko, sheria, kukutana na Wataalamu wa muziki/filamu na pia kupata elimu ya kurekodi na ku-mix muziki/filamu kwa kutumia studio zenye tekinolojia ya digitali za MSOL-AB, atakuwa amejifunza vitu vya kumwendeleza. Muziki/Filamu yake itakuwa katika kiwango cha kuridhisha zaidi kuliko hapo awali kabla ya kuja kozi MSOL- Sweden. Albamu zilizofanyiwa kazi na MSOL-AB na kupitishwa na Wasambazaji, ni marufuku kuzitengeneza tena katika Audio cassette, CD wala DVD nje ya Sweden au kwa namna yoyote bila ya ridhaa ya maandishi na MSOL-AB. Nje ya hapo ni adhabu kubwa sana itatolewa na Wanasheria wa MSOL-AB Sweden.
  7. Kwa Msanii ambaye kwa sababu hii ama ile hawezi kuja kwetu Sweden. Unaweza ku-emailing muziki wako au movies kwetu. Tuna studio ambazo MSOL-AB tuna makubaliano nao maalum Tanzania ambao wanaweza kukusaidia wewe Msanii na kukupa maelekezo namna ya kufanya shughuli hiyo ili kazi zako zisiingie kwenye mikono ya watu wasio waaminifu zikachakachuliwa na kuibiwa. Emailing muziki wako au movies kwetu ili tuweze kukutangazia kazi yako nje ya Tanzania. Kutuma demos yako kwetu, tumia E-Mail: info@msolab.se au tuma CD/DVD au Cassette kwa kutumia address ya: MSOL-AB, C/o Peters Mhoja, Ruddammsgatan 7, SE-803 20 Gävle-Sweden. Tutazipokea na sisi tutakusaidia. Usisahau kutuma mawasiliano yako ya kudumu, tuma namba ya simu yako na address yako kamili.

Kozi za MSOL-AB zitakuwa za wiki mbili hadi miezi mitatu kufuatia jinsi mshiriki atakavyo agiza (order). MSOL itakuwa ikichukua Wanamuziki aina zote wa Bongo Fleva, RnB, Hip Hop, Rock, Gospel, Zouk, Dance Taarab na wasanii wa filamu za Bongomovie na wengine wote ili kuwafanyia kazi zao kadri watakavyopendekeza wenyewe. Kwa wale ambao hawata weza kuja Sweden,watatuma kazi zao kama ilivyoelezwa hapo juu. Kama ilivyo MSOL itawashirikisha wataalam wake kuzisikiliza/kuziangali kazi hizo ili kuona ubora wa kazi zao wote. Washiriki watakaokuja Sweden wasiwe chini ya watu watatu na wasizidi watu ishirini kwa mpigo ambao watakuwa wamelipa malipo kamili ya kozi walizozitaka.

Baada ya Washiriki kukamilisha malipo yao, MSOL-AB itatumia fedha hizo kwa;-

  • Kununua tiketi zao za kwenda na kurudi Tanzania/Sweden kwa kila Mshiriki .
  • Kulipia pango la Washiriki watakapokuwa Sweden na nje ya Sweden kama watapata nafasi ya kwenda kutoa tamasha huko.
  • Gharama za chakula kwa Washiriki Sweden na kwa nchi zingine kama watapata nafasi ya kwenda kutoa tamasha huko.
  • Gharama za Walimu (Soko na Sheria) MSOL-AB itakao wakodi na madarasa tutakayoyatumia kusoma kwa Washiriki Sweden.
  • Malipo ya gharama za kuwakodisha Wataalamu wa muziki/filamu Sweden. Jopo la Majaji litakaloamua muziki/filamu ipi iendelee mbele kwa Wasambazaji. Malipo yatatofautiana kutokana na mahitaji ya Washiriki wanamiziki/wasanii wetu k.m. pop, Rock, hip pop, RnB, Gospel au Taarabu na hasa filamu maana ni muda utakuwa ukihesabika, kila Mtaalamu wa muziki MSOL-AB itampata Mtaalamu mwenye utaalamu katika fani ya muziki huo na pia katika filamu.

BongoFlava
BongoFleva ni jina lililopewa kimsingi muziki mbalimbali mikubwa kufanyika katika lugha ya Kiswahili iliyotoholewa kutoka maneno ya lugha ya kiingereza. Huu ni mchanganyiko wa Hip- Hop, Kwaito , R & B, Reggae / Dancehall , na aina nyingine ya muziki ambao unaweza kutumiwa na umeboreshwa kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili. Bongofleva linatokana na maneno mawili, ' Bongo ' ni neno la kiswahili litumiwalo na vijana kuiita Tanzania. ' Ubongo ' ambayo ina maana ya (brain) ' ubongo ' ni kawaida hutumika huwakilisha aina ngumu ya maisha Tanzania na hasa katika mji wa Da -es- salaam mtu unatakiwa kutumia "akili" ili uweze kuishi. Neno ' Flava ' ambalo maana yake ni (flavor) ' ladha '. BongoFleva ni muziki wa Tanzania wa mijini, muziki unaowakilisha muziki wa Tanzania ya leo ambao umekubalika sana ndani ya nchi.

Tanzania ilikuwa inapita katika kipindi cha ubinafsishaji na vijana wengi wamepata uwezekanaji mkubwa wa kuunganishwa na kimawasiliano na nchi zingine za dunia k.m muziki wa Hip Hop za Marekani ambayo imekuwa ni sehemu kubwa ya vijana wa Tanzania wanaitumia sana aina ya muziki huo katika kazi zao za kimuziki.

Kupanda kwa kasi ya Bongoflava , ingawa ilianza kuonyesha kukatisha tamaa, ulisababishwa na ongezeko zaidi la mahitaji kwa ajili ya kurekodi studio, na mwaka 2000 kulikaribishwa wimbi la wasanii safi ambao walitaka kufanya zaidi ya rap. Walitaka kuimba na ndivyo walivyofanya na kuimba mitindo mingine mipya, zaidi ni wale waloshiriki kuzalisha Bongoflava.Wanamuziki hawa pia waliimba juu ya nyimbo za zamani, kuhusu migogoro mbalimbali ya maisha na kuhusu mapenzi. Bongoflava waliona kushirikiana ni jambo zuri ajabu na viwanda vingine kama vile sinema na sekta ya mtindo.

Miziki mingine ni Dance and Live Band (Dansi),Taarab, Gospel (Muziki wa Injili) na Bongomovie (Filamu za Bongo).

Dance and Live Band (Dansi)
Dansi muziki pia ni maarufu sana na ina zifuatazo nzuri zaidi miongoni mwa kizazi cha zamani. Alicheza akiwa na bendi kwa fusion sauti ya Rhumba , awali kutoka Cuba na Lingala muziki awali kutoka Congo. Ingawa ni kufanywa juu ya fusions haya , ni sana inajulikana kama Jazz muziki kwa unmistaken jazz sauti na ambayo kila wimbo huanza na kabla ya upgrades , kama wewe, kwa zaidi Rhumba na Lingala sauti. Muziki Dansi ni muziki kwa ajili ya vijana kukomaa au kwa sikio kukomaa zaidi.

Taarab
Taarab muziki ni fusion ya sauti kutoka Asia ya Kusini, Afrika Kusini mwa Sahara , Afrika Kaskazini , Mashariki ya Kati na Ulaya ya kuimba katika Kiswahili utungo mashairi style. Ni ni ya kusisimua fomu ya sanaa kumpatia kutoka utamaduni classical, mkubwa maarufu kwa wanawake . Aina Taarab sehemu kubwa ya maisha ya kijamii ya Waswahili pamoja maeneo ya pwani hasa Zanzibar , Tanga na hata zaidi katika Mombasa na Malindi katika pwani ya Kenya. Wengine wanasema kuwa Taarab ni wa asili ya Misri. Legends kama Sinti Bin Saad na Bi Kidude walikuwa Taarab waimbaji maarufu zaidi.

Gospel Music
Muziki wa Injili ni kufanyika kwa twist Tanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Katika Tanzania muziki wa injili ni Ghana kuongoza ni rekodi ya mauzo na tamasha mahudhurio. Injili ni maarufu , msanii wa kwanza kupata kimataifa studio kurekodi mpango kuimba Ghana hii ya muziki.

  • Malipo ya kurekodi, ku-mix, ku-master katika studio na malipo ya Sound Engineers
  • Malipo kwa wanamuziki watakao kuwa wakipiga "Live" wakati wa ku-record na ku-mix na pia wakati wa re-mixing katika miziki iliyorekodiwa nje ya studio ya MSOL-AB. Inashauriwa kuwa producer asitumie chombo cha ki-elektroniki kutoka kwenye komputa ili kutengeneza muziki. Kwa kutumia vifaa vya ki-elektroniki kuzalisha muziki. Mtu unaweza kujikuta kuna mwenzio mwingine tayari katika pembe nyingine ya dunia alishatumia njia hiyo na chombo hicho na unajikuta muziki wako japo ungeweza kununulika ukapoteza soko, kwa vile mtu aliyetumia chombo hicho mwanzo alifanikiwa na wewe utaonekana unamgeza (copy)
  • Malipo ya Mastering kwa Mastering experts
  • Malipo ya kupata CODE maalum itakayotumika kuzitambulisha na kuzilinda miziki na filamu zisiibiwe na Maharamia duniani kote badala ya "Stickars" ambazo Msanii hwezi kuzisambaza dunia yote kumlindia kazi zake
  • Malipo ya kutengeneza albam kwa Wasambazaji. Miziki ni ile tu watakayoiona Wasambazaji kuwa imefikia kiwango hata kama haikufikia kiwango MSOL itawalipa. Pia malipo ya kutengenezea matangazo katika vituo zaidi ya elfu moja vya redio na tv duniani, magazeti na internet duniani kwa miziki au movies zilizopitishwa
  • Malipo ya kutengeneza Albamu katika studio zingine kwa ile miziki ambayo haitapasishwa na Wasambazaji katika soko la dunia na badala yake zinatengenezwa kwa ajili ya soko la ndani la Tanzania ili Washiriki wanamuziki/wasanii wasirudi Tanzania mikono mitupu. Kwa wale watakaotuma kazi zao na hazikufikia kiwango ni changa moto kwao kujitutumua zaidi katika kazi zao wajitahidi kufikia kiwango lakini isiwe ndiyo njia ya kukata tamaa na kudidimia
  • Malipo ya Mkalimani katika kipindi chote cha masomo na cha kurekodi na ku-mix kazi za wanamuziki na filamu
  • Washiriki wote watakapoomba VIZA ya kuja Sweden kwa ajili ya kozi ya MSOL-AB watapata viza zao bila usumbufu baada ya MSOL-AB kutuma orodha ya Washiriki ambao watakuwa wametoa malipo yao kamili. Malipo ya pasipoti na viza itakuwa ni juu yao Washiriki. Mipango ya baadaye ya MSOL-AB ni kujenga studio nyingine ya kisasa Tanzania, ili kurahisisha kurekodi miziki na filamu za Washiriki wa kozi kabla hawajaja Sweden, kwa sasa nitashirikiana na studio moja au mbili Tanzania ambazo nitaziamini kufanya kazi za kuridhisha na ziwe zinaaminika zisivujishe miziki au filamu kwa watu wengine ambao watafanikiwa kuendeleza kufanya uharamia wao katika kazi za wasanii wetu Tanzania na nje ambapo tunajitahidi kuwadhibiti.
  • MSOL-AB ipo tayari kushirikiana na Mashirika yanayojihusisha na wasanii na kazi zao Tanzania na nchi zingine zote duniani ili tuweze kwa pamoja kupinga ubaguzi na unyonywaji kwa wasanii maskini na wale wenye uwezo. Tuunganishe nguvu ya watu wa dunia kwa njia ya utamaduni na tusitenganishwe na utofauti wa kijiografia bila kujali lugha na utamaduni wetu, tuwe kitu kimoja.

Peters Mhoja / CEO / MSOL - AB

MSOL AB - MUSIC STUDIO OF LEARNING OF SWEDEN

Kujiunga na sisi kwenye facebook.

Admin >>